ECOBANK YAZINDUA NJIA SALAMA YA MALIPO KWA MTANDAO - FINANCIAL-24
Ecobank yaja na suluhisho la kufanya malipo salama kwa njia mtandao kupitia MASTERPASS na MVISA .Ecobank katika kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwa suluhisho kwenye sekta ya biashara ya huduma za kibenki hapa nchini leo imezindua applikesheni ya simu za mkononi itakayojulikana kama Ecobank Mobile App – MASTERPASS NA MVISA ili kusaidia wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali kufanya Malipo kwa njia rahisi na kwa usalama zaidi mahali popote.
Mtanzania yeyote ataweza kutumia teknolojia hii ya mpya ya MASTERPASS QR na MVISA kulipia gharama mbali mbali kwa kutumia simu zao za mkononi kwa kupitisha Quick Response (QR) kwa wauzaji mbalimbali wa bidhaa au watoa huduma ndani na nje ya nchi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Bi, Mwanahiba Mzee alisema “applikesheni ya Ecobank Mobile App ilizinduliwa Februari mwaka huu lakini kwa sasa imeboreshwa zaidi ili wateja wa Ecobank na wale wasio wateja wa bank hii waweze kutumia applikesheni hii duniani kote”.
‘Applikesheni ya Ecobank Mobile App ni njia rahisi ya kujipatia huduma za kibenki ndani ya nchi 33 ambazo Benki yetu inafanya biashara lakini pia unaweza kuitumia ukiwa kokote duniani. Wateja wanaweza kupakua applikesheni Ecobank Mobile App na papo hapo kujifungulia akaunti ya Ecobank kwa njia ya mtandao na kuanza kupata huduma za kibenki kama vile kufanya malipo au kuhamisha fedha bila kutembelea tawi lolote la Benki”, alisema Bi Mzee.
“Tunayo furaha kwamba applikesheni yetu ni sulushisho la huduma za haraka za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi na bado inaendea kuboreshwa zaidi na zaidi na sasa tunatumia teknolojia ya Masterpass QR na Mvisa kwa kufanya malipo mbali mbali, aliongeza.
Bi Mzee aliongeza kuwa Masterpass QR na Mvisa ni njia za mtandao (kidigitali) ambazo humfanya mteja kulipa kwa kadi ya Benki au akaunti zake za benki ambazo pia zimeunganishwa katika mtandao huu kwa kugusisha na kufanya malipo. ‘Hii ni njia ya kutumia simu za mkononi ambapo mnunuzi ataweza kumlipa muuzaji au mtoa huduma yeyote na hivyo inakuwa ni suluhisho kwa wajasiriamli wadogo, wa kati na wakubwa’, aliongeza Bi Mzee.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi Swere Ndabu alisema “Ili kutumia huduma hii wateja wa Ecobank na wasio wateja wa Ecobank wanatakiwa kupakua Applikesheni ya Ecobank Mobile App kwenye smartphone zao kisha wanajisajili kwa kutumia kadi ya Visa au Master , au kufungua akaunti ya Ecobank Xpress papo hapo na kuanza kufanya miamala ya malipo. Kwa wale ambao ni wateja wanatakiwa kupakua na kuanza kutumia applikesheni kwa kutumia debit card au Ecobank Retail internet banking.”
“Kwa kutumia applikesheni hii wakati wa kufanya Malipo, mteja atanufaika kwa kuokoa muda wake na kupunguza gharama za kutembelea tawi la Benki, ataweza pia kufanya Malipo kwa haraka na kwa usalama zaidi pamoja na kuongeza mauzo kwa vile njia hii itachochea matumizi au manunuzi salama. Vilevile itamsaidia muuzaji sana kwani ni njia rahisi ya kutunza kumbu kumbu za mauzo.” alisema Swere.
Swere aliongeza kuwa kwa kutumia applikesheni ya Ecobank Mobile App mteja anaweza akahamisha fedha kwenye akaunti yake ya Ecobank akiwa hapa nchini au nje ya Tanzania, pia ataweza kuhamisha fedha kwenda Benki nyingine hapa nchini au kwenda kwenye kadi za Visa duniani kote na pia kwenye mitandao ya simu za mkononi ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.
This is the article ECOBANK YAZINDUA NJIA SALAMA YA MALIPO KWA MTANDAO - FINANCIAL-24 this time, hopefully can benefit for you all. well, see you in other article post.
Title : ECOBANK YAZINDUA NJIA SALAMA YA MALIPO KWA MTANDAO - FINANCIAL-24
link : ECOBANK YAZINDUA NJIA SALAMA YA MALIPO KWA MTANDAO - FINANCIAL-24
0 Response to "ECOBANK YAZINDUA NJIA SALAMA YA MALIPO KWA MTANDAO - FINANCIAL-24"
Post a Comment